Nokia 6600 slide - Taarifa ya betri na chaja

background image

Taarifa ya betri na chaja
Kifaa chako kinatumia betri inayoweza kuchajiwa upya. Betri

iliyokusudiwa kutumiwa na kifaa hiki ni BL-4U. Kifaa hiki

kimekusudiwa kutumika kinapopokea umeme kutoka kwa

chaja zifuatazo: AC-8. Betri inaweza kuchajiwa na

kuondolewa chaji hata mara mia, lakini hatimaye itachoka.

Wakati muda wa kuongea na muda wa kusubiri unaonekana

wazi kuwa mfupi kuliko kawaida, badilisha betri. Tumia betri

zilizoidhinishwa tu na Nokia, na weka chaji kwenye betri

yako kwa kutumia chaja zilizoidhinishwa tu na Nokia kwa

ajili ya kifaa hiki. Utumiaji wa betri au chaja isiyoidhinishwa

inaweza kuleta hatari ya moto, mlipuko, uvujaji, au hatari

zingine.

Namba halisi ya modeli ya chaja inaweza kutofautiana

kulingana na aina ya plagi. Utofauti wa plagi unatambuliwa

na moja ya yafuatayo: E, EB, X, AR, U, A, C, au UB.

Ikiwa betri inatumiwa kwa mara ya kwanza au ikiwa betri

haijatumika kwa muda mrefu, inaweza kuwa lazima

kuunganisha chaja, halafu kukata unganisho na kuunganisha

tena ili kuanza kuchaji betri. Kama betri imeishiwa chaji

kabisa, inaweza kuchukua dakika kadhaa kabla kiashirio cha

kuchaji hakijatokea kwenye simu au kabla simu zozote

kuweza kupigwa.

Daima zima kifaa na ondoa unganiko kwenye chaja kabla ya

kuondoa betri.

Chomoa unganiko la chaja kwenye plagi ya umeme na

kwenye kifaa wakati hakitumiki. Usiache betri iliyochajiwa

kabisa ikiwa imeunganishwa kwenye chaja, kwa sababu

uwekaji wa chaji ya ziada kunaweza kufupisha maisha yake.

Ikiachwa bila kutumika, betri iliyokuwa imejaa chaji

itapoteza chaji yake kadri muda unavyopita.

Daima jaribu kuweka betri kwenye halijoto kati ya 15°C na

25°C (59°F na 77°F). Halijoto ya juu sana hupunguza uwezo

na uhai wa betri. Kifaa chenye betri moto au baridi kinaweza

kisifanye kazi kwa muda. Ufanyaji kazi wa betri unapungua

sana kwenye halijoto zilizo chini ya kiwango cha kuganda.

Usifanye mkato wa umeme kwenye betri. Mkato wa umeme

unaweza kutokea kwa bahati mbaya kama kitu cha chuma

kama sarafu, klipu au kalamu kimesababisha kuunganisha

temino za chanya (+) na hasi (–) za betri. (Hivi huonekana

kama vipapi vya chuma kwenye betri.) Hii inaweza kutokea,

kwa mfano, wakati ukibeba betri ya akiba mfukoni mwako

au kwenye pochi. Mkato wa umeme kwenye temino huweza

kuharibu betri au hicho kinachounganisha.

Usitupe betri zilizokwishatumika kwenye moto kwa sababu

zinaweza kulipuka. Betri zinaweza pia kulipuka kama

zimeharibika. Tupa betri kwa kufuata sheria za mahali ulipo.

Tafadhali rejeleza betri pale inapowezekana. Usitupe kama

takataka za kawaida za nyumbani.

Usimamiaji haki za kidijito (‘Digital rights management’) 41

background image

Usichanechane, kukata, kufungua, kugongesha, kukunja,

kuharibu, kutoboa au kupasua seli au betri. Katika tukio la

betri kuvuja, usiruhusu kimiminika kugusana na ngozi au

macho. Kwenye tukio la uvujaji wa aina hiyo, osha ngozi au

macho yako mara moja na maji, au tafuta msaada wa

kitabibu.

Usirekebishe, kutengeneza tena, kujaribu kuingiza vitu geni

kwenye betri, au kuingiza au kuweka wazi kwa maji au

umiminiko mwingine.

Utumiaji betri vibaya kunaweza kusababisha moto, mlipuko

au hatari zingine. Kifaa au betri kikiangushwa, haswa kwa

sakafu ngumu, na unaamini betri imeharibika, ipeleke kwa

kituo cha huduma ifanyiwe uchunguzi kabla ya kuendelea

kuitumia.

Tumia betri kwa matumizi yaliyokusudiwa tu. Kamwe

usitumie chaja yoyote au betri iliyoharibika. Weka betri mbali

na mahali watoto wadogo wanapoweza kufika.