Nokia 6600 slide - Huduma za mtandao

background image

Huduma za mtandao

Ili uweze kutumia simu unahitajika kuwa

na huduma kutoka kwa mtoa huduma wa

vifaa visivyotumia waya. Vitendaji vingi

huhitaji vitendaji maalumu vya mtandao.

Vitendaji hivi havipatikani kwenye

mitandao yote; mitandao mingine

inaweza kuhitaji kufanya mipango

mahususi na mtoa huduma wako kabla

hujaweza kutumia huduma za mtandao.

Mtoa huduma wako anaweza kukupa

maelekezo na kueleza gharama zipi

zitakazotumika. Baadhi ya mitandao

inaweza kuwa na vikomo ambavyo

vinaweza kuathiri namna unavyoweza

kutumia huduma za mtandao. Kwa mfano

baadhi ya mitandao inawezekana

isiendane na herufi na tarakimu zote za

lugha fulani.
Mtoa huduma wako anaweza kuwa

ameomba kwamba vitendaji fulani

vifanywe visifanye kazi au visiwekwe

tayari kwenye kifaa chako. Kama ni hivyo,

vitendaji hivyo havitatokea kwenye

menyu ya kifaa chako. Kifaa chako

kinaweza pia kuwa na upangiaji maalumu

kama vile mabadiliko kwenye majina ya

menyu, mfuatano wa menyu na alama.

Wasiliana na mtoa huduma wako kwa

taarifa zaidi.