Ingiza SIM kadi na betri
Daima zima kifaa na ondoa unganiko
kwenye chaja kabla ya kuondoa betri.
Simu hii inakusudiwa kutumiwa na betri
ya BL-4U. Daima tumia betri asili za Nokia.
Angalia Mwongozo wa jinsi ya kutambua
betri za Nokia. uk. 42.
SIM kadi na anwani zake zinaweza
kuharibiwa kirahisi na mikwaruzo au
mikunjo, kwahivyo uwe mwangalifu
unaposhika, unapoingiza au kutoa kadi
hiyo.
1 Sukuma kitufe cha kuachilia, na
ufungue kifuniko cha nyuma. Ondoa
betri.
2 Fungua kishikilia SIM kadi. Ingiza SIM
kadi kwa kishika eneo la mguso
likiangalia chini. Funga kishika SIM
kadi.
3 Zingatia miguso ya betri, na uingize
betri. Rudisha kifuniko cha nyuma.
6
Ifanye iwe simu yako