Nokia 6600 slide -  Kuhusu simu yako 

background image

Kuhusu simu yako

Kifaa kisichotumia waya kilichoelezwa

kwenye mwongozo huu kimeidhinishwa

kutumika kwenye WCDMA 850 na 2100 na

GSM 850, 900, 1800, na 1900. Wasiliana na

mtoa huduma wako ili upate taarifa zaidi

kuhusu mitandao.
Wakati ukitumia vitendaji kwenye kifaa

hiki, tii sheria zote na heshimu utamaduni

wa wenyeji, uhuru binafsi wa mtu na haki

halali za wengine, ikiwemo hakimiliki.
Kinga za hakimiliki zinaweza kuzuia

baadhi ya picha, muziki na vitu vingine

visinakiliwe, kurekebishwa au

kuhamishwa.
Kifaa chako kinaweza kuwa na vialama

vilivyosakinishwa mapema na viungo vya

tovuti vya mtu mwingine. Unaweza

kufikia tovuti zingine za mtu mwingine

kupitia kifaa chako tu. Tovuti za mtu

mwingine hazishirikiani na Nokia, na

Nokia haiidhinishi wala kutoa dhamana

kwa ajili ya tovuti hizo. Ukiamua kufikia

tovuti hizo, unapaswa kuwa mwangalifu

kwa usalama au vilivyomo.

8

Ifanye iwe simu yako

background image

Tahadhari:

Ili kutumia vitendaji vyovyote kwenye

kifaa hiki, isipokuwa saa ya kengele, kifaa

hicho lazima kiwe kimewashwa.

Usiwashe kifaa wakati matumizi ya kifaa

kisichotumia waya yanaweza

kusababisha mwingiliano au hatari.

Kumbuka kutengeneza nakala za

kumbukumbu kwa dharura au kuweka

kumbukumbu ya maandishi kwa ajili ya

taarifa zote zilizohifadhiwa kwenye kifaa

chako.
Wakati ukiunganisha na kifaa chochote

kingine, soma mwongozo wake wa

mtumiaji upate maelezo ya kina kuhusu

usalama. Usiunganishe bidhaa ambazo

haziendani.
Muhimu: Tumia huduma zile tu ambazo

unaziamini na ambazo hutoa usalama na

ulinzi wa kutosha dhidi ya maunzi laini

yenye madhara.