
Rejesha mipangilio ya kiwandani
Kurejesha simu kwa hali ya kiwandani,
chagua
Menyu
>
Mipangilio
>
Rej. mip.
k'anda.
na kutoka kwa ifuatayo:
Rejesha mip'ngilio tu — Kubadili
mipangilio yote iliyopendekezwa bila
kufuta data yote ya kibinafsi
Rejesha zote — Kubadili mipangilio yote
iliyopendekezwa na kufuta data yote ya
kibinafsi kama majina, taarifa na faili za
wasiliano.
40 Msaada na visasisho vya programu ya simu

Usimamiaji haki za kidijito (‘Digital rights
management’)
Wamiliki wa vilivyomo wanaweza kutumia aina tofauti za
teknolojia za usimamiaji haki za kidijito (‘usimamiaji haki za
dijiti’ - DRM) kulinda haki zao za ubunifu, zikiwemo
hakimiliki. Kifaa hiki kinatumia aina anuai za maunzi laini ya
DRM ili kuingia kwenye vitu vinavyolindwa na DRM. Ukiwa na
kifaa hiki unaweza kufikia vilivyomo vilivyolindwa na
WMDRM 10, OMA DRM 1.0, OMA DRM 1.0 kifuli cha mbele, na
OMA DRM 2.0. Ikiwa baadhi ya maunzi laini ya DRM
yameshindwa kulinda vilivyomo, wamiliki wa vilivyomo
wanaweza kuomba kwamba uwezo wa maunzi laini hayo ya
DRM ya kuingia kwenye vitu vipya vinavyolindwa na DRM
ubatilishwe. Ubatilishwaji huo unaweza pia kuzuia uwekwaji
upya wa vitu vinavyolindwa na DRM ambavyo tayari viko
kwenye kifaa chako. Ubatilishwaji wa maunzi laini hayo ya
DRM hauathiri matumizi ya vitu vinavyolindwa na aina
nyingine za DRM au matumizi ya vitu visivyolindwa na DRM.
Vitu vinavyolindwa na usimamiaji haki za kidijito ('Digital
rights management –DRM') huja na kifungulio ambacho
huainisha haki zako za kutumia vilivyomo.
Ikiwa kifaa chako kina yaliyomo yaliyolindwa ya OMA DRM, ili
kuweka nakala za kumbukumbu za vifunguo vya kuamilisha
na yaliyomo, tumia kitendaji cha kuweka nakala za
kumbukumbu kwenye Nokia PC Suite. Namna nyingine za
uhamishaji huenda zisihamishe vifungulio ambavyo
vinahitaji kurejeshwa na vilivyomo ili uweze kuendelea na
matumizi ya vitu vinavyolindwa na OMA DRM- baada ya
kumbukumbu ya kifaa kufomatiwa. Unaweza pia kuhitaji
kurejesha vifungulio inapotokea kuwa mafaili kwenye kifaa
chako yameharibiwa.
Kama kifaa chako kina vitu vinavyolindwa na WMDRM,
vifungulio na vilivyomo vinaweza kupotea kama
kumbukumbu ya kifaa ikifomatiwa. Unaweza pia kupoteza
vifungulio na vilivyomo ikiwa mafaili ya kwenye kifaa chako
yakiharibiwa. Kupoteza vifungulio au vilivyomo kunaweza
kupunguza uwezo wako wa kutumia vilivyomo vilevile
kwenye kifaa chako tena. Kwa taarifa zaidi, wasiliana na
mtoa huduma wako.
Nyongeza
Tahadhari:
Tumia betri, chaja, na vifaa vya nyongeza ambavyo
vimeidhinishwa na Nokia kwa ajili ya matumizi na modeli hii
tu. Matumizi ya aina nyingine yanaweza kubatilisha
uthibitisho au dhamana yoyote, na inaweza kuwa hatari.
Kuhusu upatikanaji wa vifaa vya nyongeza vilivyoidhinishwa,
tafadhali mwulize muuzaji wako. Unapoondoa waya ya
umeme kwenye kifaa chochote cha nyongeza, kamata na
uvute plagi na siyo waya.
Betri
Taarifa ya betri na chaja
Kifaa chako kinatumia betri inayoweza kuchajiwa upya. Betri
iliyokusudiwa kutumiwa na kifaa hiki ni BL-4U. Kifaa hiki
kimekusudiwa kutumika kinapopokea umeme kutoka kwa
chaja zifuatazo: AC-8. Betri inaweza kuchajiwa na
kuondolewa chaji hata mara mia, lakini hatimaye itachoka.
Wakati muda wa kuongea na muda wa kusubiri unaonekana
wazi kuwa mfupi kuliko kawaida, badilisha betri. Tumia betri
zilizoidhinishwa tu na Nokia, na weka chaji kwenye betri
yako kwa kutumia chaja zilizoidhinishwa tu na Nokia kwa
ajili ya kifaa hiki. Utumiaji wa betri au chaja isiyoidhinishwa
inaweza kuleta hatari ya moto, mlipuko, uvujaji, au hatari
zingine.
Namba halisi ya modeli ya chaja inaweza kutofautiana
kulingana na aina ya plagi. Utofauti wa plagi unatambuliwa
na moja ya yafuatayo: E, EB, X, AR, U, A, C, au UB.
Ikiwa betri inatumiwa kwa mara ya kwanza au ikiwa betri
haijatumika kwa muda mrefu, inaweza kuwa lazima
kuunganisha chaja, halafu kukata unganisho na kuunganisha
tena ili kuanza kuchaji betri. Kama betri imeishiwa chaji
kabisa, inaweza kuchukua dakika kadhaa kabla kiashirio cha
kuchaji hakijatokea kwenye simu au kabla simu zozote
kuweza kupigwa.
Daima zima kifaa na ondoa unganiko kwenye chaja kabla ya
kuondoa betri.
Chomoa unganiko la chaja kwenye plagi ya umeme na
kwenye kifaa wakati hakitumiki. Usiache betri iliyochajiwa
kabisa ikiwa imeunganishwa kwenye chaja, kwa sababu
uwekaji wa chaji ya ziada kunaweza kufupisha maisha yake.
Ikiachwa bila kutumika, betri iliyokuwa imejaa chaji
itapoteza chaji yake kadri muda unavyopita.
Daima jaribu kuweka betri kwenye halijoto kati ya 15°C na
25°C (59°F na 77°F). Halijoto ya juu sana hupunguza uwezo
na uhai wa betri. Kifaa chenye betri moto au baridi kinaweza
kisifanye kazi kwa muda. Ufanyaji kazi wa betri unapungua
sana kwenye halijoto zilizo chini ya kiwango cha kuganda.
Usifanye mkato wa umeme kwenye betri. Mkato wa umeme
unaweza kutokea kwa bahati mbaya kama kitu cha chuma
kama sarafu, klipu au kalamu kimesababisha kuunganisha
temino za chanya (+) na hasi (–) za betri. (Hivi huonekana
kama vipapi vya chuma kwenye betri.) Hii inaweza kutokea,
kwa mfano, wakati ukibeba betri ya akiba mfukoni mwako
au kwenye pochi. Mkato wa umeme kwenye temino huweza
kuharibu betri au hicho kinachounganisha.
Usitupe betri zilizokwishatumika kwenye moto kwa sababu
zinaweza kulipuka. Betri zinaweza pia kulipuka kama
zimeharibika. Tupa betri kwa kufuata sheria za mahali ulipo.
Tafadhali rejeleza betri pale inapowezekana. Usitupe kama
takataka za kawaida za nyumbani.