
Huduma za ziada
Unaweza kuboresha ramani na
urambazaji unaoongozwa na sauti,
ambayo inahitaji leseni ya eneo. Kutumia
huduma hii, unahitaji kifaa cha nje cha
GPS kinachoendana ambacho kinakubali
teknolojia ya Bluetooth isiotumia waya.
Kununua huduma ya urambazaji ilio na
uogozi wa sauti, chagua
Menyu
>
Ramani
>
Huduma za ziada
>
Nunua
urambazaji
, na ufuate maagizo.
Kutumia urambazaji na uongozi wa sauti,
lazima uruhusu programu-tumizi ya
Ramani kutumia unganisho la mtandao.
Leseni ya urambazaji imeunganishwa
kwa SIM kadi yako. Ukiingiza SIM kadi
nyingine kwenye simu yako, unaulizwa
ununue leseni unapoanza urambazaji.
Wakati wa utaratibu wa ununuzi,
unaulizwa kuhawilisha leseni ya
urambazaji ya sasa kwa SIM kadi mpya
bila malipo yoyote.
Je, unajua kwamba
unaweza kusimamia
muziki yako, majina na
kalenda kati ya simu yako na
kompyuta yako na Nokia PC
Suite?