Ramani na GPS
Unaweza kutumia mfumo wa kijumla wa
mkao (GPS) ili kusaidia programu-tumizi
ya Ramani. Pata eneo lako, au pima
umbali na ratibu.
Kabla uweze kutumia kitendaji cha GPS,
lazima ulinganishe simu yako na kipokea
GPS cha nje kinachoendana kwa kutumia
teknolojia ya Bluetooth isiotumia waya.
Kwa habari zaidi, angalia kiongozi cha
mtumiaji cha kifaa chako cha GPS.
Baada ya kulinganisha kifaa cha Bluetooth
cha GPS na simu, inaweza kuchukua
Ramani 33
dakika kadhaa kwa simu kuonyesha eneo
la sasa. Maunganisho yafuatayo
yanastahili kuwa ya kasi, lakini kama
hujatumia GPS kwa siku kadhaa, au uko
mbali sana na pahali pa mwisho
ulipoitumia, inaweza kuchukua dakika
kadhaa kugundua na kuonyesha eneo
lako.
Mfumo wa Utambuzi wa Mahali Ulipo
Duniani {The Global Positioning System
(GPS)} huendeshwa na serikali ya
Marekani (USA), ambayo ndiyo pekee
inayowajibika na usahihi na utunzaji
wake. Usahihi wa data ya mahali ulipo
unaweza kuathiriwa na marekebisho
yanayofanywa kwenye setelaiti za GPS
unaofanywa na Serikali ya Marekani na
unaweza kubadilika kutokana na sera ya
kiraia ya GPS ya idara ya Kimarekani
ijulikanayo kama ‘United States
Department of Defense’ na mpango
ujulikanao kama ‘Federal
Radionavigation Plan’. Usahihi unaweza
pia kuathiriwa na uwekwaji au ukaaji
mbaya wa setelaiti. Upatikanaji na ubora
wa ishara za GPS unaweza kuathiriwa na
mahali ulipo, majengo, vizuizi vya asili na
hali ya hewa. Kipokeaji cha GPS kinapaswa
kutumika daima nje ya majengo ili
kuruhusu upatikanaji wa ishara za GPS.
GPS yoyote isitumiwe kwa ajili ya vipimo
vya uhakika sana kuhusu ulipo na kamwe
usitegemee tu taarifa za mahali ulipo
kutoka kwenye kipokeaji cha GPS na
mitandao ya selula ya redio kwa ajili ya
kujua mahali ulipo au kuongozea.