Nokia 6600 slide - Magari

background image

Magari
Mawimbi ya redio (RF) yanaweza kuathiri mifumo ya eletroni

iliyo ndani ya gari ambayo imewekwa vibaya au haijalindwa

kikamilifu, kwa mfano mifumo ya eletroni ya mdungo wa

mafuta; mifumo ya elektoni ya kufunga breki yenye kuzuia

utelezi (kutokujifunga); ya eletroni ya kusimamia mwendo,

ya mifuko ya hewa. Kwa taarifa zaidi, wasiliana na

watengenezaji au wawakilishi wa gari lako au kifaa chochote

ambacho kimeongezwa.

Watu wenye sifa zinazostahili tu ndio wanapaswa kufanyia

matengenezo kifaa hiki au kukiweka ndani ya gari. Uwekaji

au utengenezaji wenye makosa unaweza kuwa wa hatari na

Taarifa ya nyongeza kuhusu usalama 43

background image

kunaweza kubatilisha dhamana yoyote ambayo inaweza

kuwepo kwa ajili ya kifaa. Kagua mara kwa mara kwamba

vifaa vyote visivyotumia waya ndani ya gari vimefungwa

vizuri na vinafanya kazi sawasawa. Usihifadhi au kubeba

vimiminika vinavyoweza kuwaka, gesi au vitu vyenye

kulipuka kwenye kichumba kimoja na kifaa hiki, sehemu zake

au vifaa vyake vya nyongeza. Kwa magari yenye mifuko ya

hewa, kumbuka kwamba mifuko ya hewa hujaa hewa kwa

nguvu kubwa. Usiweke vitu, pamoja na vilivyofungwa au

vifaa vinavyohamishika visivyotumia waya kwenye eneo juu

ya mfuko wa hewa au kwenye eneo ambalo mfuko wa hewa

hutumika. Kama vifaa visivyotumia waya vya ndani ya gari

vimewekwa vibaya na mfuko wa hewa ukajaa hewa,

madhara makubwa yanaweza kutokea.

Kutumia kifaa chako ukiwa ndani ya ndege inayoruka hewani

kumepigwa marufuku. Zima kifaa chako kabla ya kupanda

ndege. Matumizi ya vifaa vya umeme visivyotumia waya

ndani ya ndege yanaweza kuwa hatari kwa ufanyaji kazi wa

ndege, kuharibu mtandao wa simu za upepo na inaweza

kuwa ni uvunjaji wa sheria.