
Mazingira ya kutumia
Kifaa hiki kinatimiza matakwa ya maelekezo ya ujiwekaji
wazi kwa frikwensi za redio wakati kikitumika ama kwenye
mkao wa kawaida kwenye sikio au wakati kikiwekwa
angalau Sentimita 1.5 (inchi 5/8) kutoka kwenye mwili.
Wakati kikasha cha kubebea, kishikiza kwenye mkanda au
kishikizi kikitumika kwa matumizi ya kuvaliwa mwilini,
kinatakiwa kisiwe na chuma na kinatakiwa kuweka bidhaa
hii angalau umbali uliotajwa hapo juu kutoka kwenye mwili
wako.
Kupitisha mafaili ya data au ujumbe, kifaa hiki kinahitaji
unganiko na mtandao wenye ubora wa hali ya juu. Wakati
mwingine, upitishaji wa mafaili ya data au ujumbe unaweza
kucheleweshwa hadi unganiko hilo litakapopatikana.
Hakikisha kwamba umbali wa utenganisho wa hapo juu
unafuatwa mpaka upitishaji ukamilike.