
Mazingira yenye uwezekano wa milipuko
Zima kifaa chako katika eneo lenye mazingira yenye
uwezekano wa milipuko na tii ishara na maelekezo yote
Mazingira yenye uwezekano wa milipuko yanajumuisha
maeneo ambayo kwa kawaida ungeshauriwa kuzima injini
ya gari lako. Cheche katika maeneo kama hayo zinaweza
kusababisha mlipuko au moto unaoweza kuleta majeraha ya
mwili au hata kifo. Zima kifaa chako kwenye vituo vya
kuongeza mafuta kama vile karibu na pampu za gesi kwenye
vituo vya kuongeza mafuta. Fuata masharti ya kuzuia
matumizi ya vifaa vya redio kwenye depo za mafuta, maeneo
ya kuhifadhi na kugawia mafuta, viwanda vya kemikali au
mahali ambapo shughuli za ulipuaji zinaendelea kufanyika.
Maeneo yenye mazingira yenye uwezekano wa milipuko
mara nyingi lakini si mara zote yanakuwa na alama zilizo
wazi. Inajumuisha chini ya sitaha ya boti, maeneo ya
usafirishaji au ya kuhifadhi kemikali na maeneo ambayo
hewa ina kemikali au chembechembe kama vile nafaka,
vumbi au poda ya chuma. Unapaswa kuwasiliana na
watengenezaji wa magari yanayotumia mafuta aina ya gesi
oevu ya petroli iliyoyeyushwa (kama vile propeni au buteni);
ili kuamua ikiwa kifaa hiki kinaweza kutumiwa vizuri katika
maeneo yao.