Nokia 6600 slide - Simu za dharura

background image

Simu za dharura
Muhimu:
Kifaa hiki hufanya kazi kwa kutumia mawimbi ya

redio, mitandao isiyotumia waya, mitandao ya ardhini, na

vitendaji vilivyowekwa na mtumiaji. Ikiwa kifaa chako

kinaruhusu simu za sauti za tovuti (simu za tovuti), anzisha

simu za tovuti na simu ya selula. Kifaa kitajaribu kupiga simu

ya dharura kwa mitandao ya selula na kupitia mtoa huduma

wako wa simu ya tovuti ikiwa zote zimeakishwa. Unganisho

katika hali zote haziwezi kuhakikishwa. Usitegemee kifaa

chochote kisichotumia waya pekee kwa mawasiliano

muhimu kama dharura za tiba.

Kupiga simu ya dharura:

1

Kama kifaa kimezimwa, kiwashe. Angalia kama kuna

mawimbi ya simu ya kutosha. Ikitegemea na kifaa

chako, pia unaweza kuhitaji kukamilisha yafuatayo:

Ingiza SIM kadi ikiwa kifaa chako kinaitumia.

Ondoa vizuizi fulani vya simu ambavyo

umeamilisha katika kifaa chako.

Badilisha mfumo wako kutoka kwa nje ya

mkondo au modi ya mfumo wa ndege hadi kwa

mfumo unaotumika.

2

Bonyeza kitufe cha kuzima simu mara nyingi kadiri

inavyohitajika ili kusafisha kinachooneshwa na

kuweka kifaa tayari kwa ajili ya kupiga na kupokea

simu.

3

Ingiza namba rasmi ya dharura ya eneo ulipo wakati

huo. Namba za dharura hutofautiana kimaeneo.

4

Bonyeza kitufe cha kupiga simu.

Wakati wa kupiga simu ya dharura, toa taarifa zote muhimu

kwa usahihi kadri inavyowezekana. Kifaa chako kisichotumia

waya kinaweza kuwa ndiyo njia pekee ya mawasiliano

kwenye tukio la ajali. Usikate simu mpaka upewe ruhusa ya

kufanya hivyo.