TAARIFA JUU YA VYETI (SAR)
Kifaa hiki cha mkononi kinatimiza maelekezo
yanayohusu ujiwekaji wazi kwa mawimbi ya redio.
Kifaa chako cha mkononi ni transmita na kipokezi cha redio.
Imesanifiwa isizidi viwango vya juu vya ujiwekaji wazi kwa
nishati ya frikwensi za redio vilivyopendekezwa na
maelekezo ya kimataifa. Maelekezo haya yalitayarishwa na
shirika huru la kisayansi ICNIRP na yanajumuisha viwango
vya tahadhari ya ziada iliyowekwa kuhakikisha usalama wa
watu wote, bila kujali umri wala afya.
Maelekezo ya ujiwekaji wazi kwa ajili ya vifaa vya mkononi
hutumia kizio cha kipimo kijulikanacho kama Kiwango
Maalum cha Ufyonzaji ( ‘Specific Absorption Rate, au SAR’ ).
Kiwango cha juu cha ‘SAR’ kilichoelezwa kwenye maelekezo
hayo ya ICNIRP ni 2.0 wati/kilogramu (W/kg) kilichotokana na
wastani wa gramu 10 za tishu. Vipimo kwa ajili ya ‘SAR’
hufanyika kwa kutumia mikao ya matumizi ya kawaida na
kifaa kikiwa kinatumika kwa kiwango chake cha juu cha
nguvu kilichosajiliwa kwenye frikwensi za bendi zote
zilizojaribiwa. Kiwango halisi cha ‘SAR’ cha kifaa wakati
kinatumika kinaweza kuwa chini ya kiwango cha juu kabisa
kwa sababu kifaa kimesanifiwa kutumia kiasi kile cha nguvu
inayohitajika tu kufika kwenye mtandao. Kiasi hicho
hubadilika kutegemea sababu kadhaa kama vile ukaribu wa
kituo cha mtandao. Kiwango cha juu cha SAR kwenye
maelekezo ya ICNIRP wakati wa kutumia kifaa karibu na sikio
ni 0.44 W/kg .
Matumizi ya vifaa vya ziada na vya nyongeza yanaweza
kusababisha viwango tofauti vya SAR. Viwango vya ‘SAR’
44 Taarifa ya nyongeza kuhusu usalama
vinaweza kutofautiana kutegemea matakwa ya nchi kuhusu
utoaji taarifa na upimaji na bendi ya mtandao. Taarifa zaidi
kuhusu SAR inaweza kupatikana chini ya taarifa ya bidhaa
kwenye www.nokia.com.
Taarifa ya nyongeza kuhusu usalama 45