
Vifaa vya tiba
Utumiaji wa kifaa chochote kinachotoa mawimbi ya redio,
ikiwa ni pamoja na simu zisizotumia waya, kunaweza
kuingiliana na utendakazi wa vifaa vya kitabibu ambavyo
havijalindwa kikamilifu. Mwone daktari au mtengenezaji wa
kifaa hicho cha kitabibu kujua kama vimelindwa kikamilifu
dhidi ya nishati ya mawimbi ya redio (RF) ya nje au kama una
maswali yoyote. Zima kifaa chako katika vituo vya afya kama
sheria zilizobandikwa kwenye maeneo hayo zinakutaka
ufanye hivyo. Hospitali au vituo vya afya vinaweza kuwa
vinatumia vifaa ambavyo vinaathirika na nishati ya mawimbi
ya nje ya redio (RF)
Vifaa vya tiba
Watengenezaji wa vifaa vya matibabu hupendekeza kwamba
utenganisho wa angalau sentimeta 15.3 (inchi 6) uwekwe
kati ya kifaa kisichotumia waya na kifaa cha matibabu
mwilini, kama vile kirekebisha mapigo ya moyo na vifaa
vingine vinavyohusiana na moyo ili kuepuka uwezekano wa
mwingiliano na kifaa hicho cha kimatibabu. Watu ambao
wana vifaa kama hivyo wanapaswa:
•
Daima kuweka kifaa hicho kisichotumia waya zaidi ya
sentimeta 15.3 (inchi 6) kutoka kwa kifaa cha matibabu
wakati kifaa kisichotumia waya kinapowashwa.
•
Wasibebe kifaa kisichotumia waya kwenye mfuko wa
shati.
•
Watumie kifaa kisichotumia waya kwenye sikio la
upande ulio mkabala na kifaa cha matibabu ili
kupunguza uwezekano wa mwingiliano.
•
Zima kifaaa kisichotumia waya mara moja ikiwa kuna
sababu yoyote ya kushuku kwamba mwingiliano
unafanyika.
•
Soma na ufuate maagizo kutoka kwa mtengenezaji wa
kifaa cha matibabu mwilini.
Ikiwa una maswali yoyote kuhusu kutumia kifaa chako
kisichotumia waya na kifaa cha matibabu mwilini, wasiliana
na mtoa huduma wako wa afya.