
Utunzaji na ukarabati
Kifaa chako ni bidhaa ya usanifu na utengenezaji wa hali ya
juu sana na kinapaswa kitumike kwa uangalifu.
Mapendekezo yafuatayo yatakusaidia kulinda matakwa ya
dhamana yako.
•
Weka kifaa kikiwa kikavu. Taka za mtuamo, unyevu wa
hewa na aina zote za vimiminiko au unyevu zinaweza
kuwa na madini yanayoweza kutia kutu saketi za
elektroniki. Kifaa chako kikilowana, ondoa betri na
kiruhusu kifaa kikauke kabisa kabla ya kurudisha betri
tena.
•
Usitumie au kuhifadhi kifaa chako kwenye maeneo
yenye vumbi na uchafu. Sehemu zake zinazosogea na
vijenzi vya elektroniki vinaweza kuharibika.
•
Usihifadhi kifaa kwenye maeneo yenye joto. Joto la juu
linaweza kufupisha maisha ya vifaa vya elektroniki,
kuharibu betri, na kukunja au kuyeyusha aina fulani za
plastiki.
•
Usihifadhi kifaa kwenye maeneo ya baridi. Wakati
kimerudi kwenye joto lake la kawaida, unyevunyevu
unaweza kutengenezeka ndani ya kifaa, ambao
unaweza kuharibu bodi za saketi za eletroni.
•
Usijaribu kufungua kifaa zaidi ya jinsi ilivyoelekezwa
kwenye mwongozo huu.
•
Usiangushe, kugonga au kutikisa kifaa hiki. Ushikwaji
ovyo unaweza kuvunja bodi za saketi na mashine
nadhifu zilizo ndani.
•
Usitumie kemikali kali, visafishaji kwa kuyeyusha, au
sabuni kali kusafisha kifaa hiki.
•
Usipake rangi kifaa. Rangi inaweza kuziba sehemu zake
zinazosogea na kuzuia utendaji kazi mzuri.
•
Tumia kitambaa laini, kisafi na kikavu kusafisha lenzi
zozote kama vile lenzi za kamera, kitambuzi cha umbali
na kitambuzi cha mwanga.
•
Tumia antena uliyopewa na simu au ukibadilisha tumia
iliyoidhinishwa tu. Antena, kufanya mabadiliko au
kuweka viambatisho visivyoidhinishwa kunaweza
kuharibu kifaa hiki na kunaweza kukiuka sheria
zinazoendana na vifaa vya redio.
•
Tumia chaja ndani ya nyumba.
•
Daima weka nakala za dharura za data ambayo unataka
kutunza, kama vile majina na miadi ya kalenda.
42 Mwongozo wa jinsi ya kutambua betri za Nokia.

•
Ili kuweka upya kifaa mara kwa mara kwa ajili ya
kupata utendaji mzuri zaidi, zima kifaa halafu ondoa
betri.
Mapendekezo haya yanahusu kwa usawa kifaa chako, betri,
chaja au kifaa chochote cha nyongeza. Kama kifaa chochote
hakifanyi kazi sawasawa, kipeleke kwenye kitengo cha
mtengenezaji aliyeidhinishwa kilicho karibu ili kihudumiwe.