Piga simu ya video
Katika simu ya video, video iliorekodiwa
na kamera ya mbele kwenye simu yako
huonyeshwa kwa mpokea simu ya video.
Kupiga simu ya video, lazima uwe na kadi
ya USIM na uwe umeunganishwa kwa
mtandao wa WCDMA. Kwa upatikanaji na
kujiandikisha kwa huduma za simu ya
video, wasiliana na opereta wa mtandao
wako. Simu ya video inaweza kupigwa
kwa simu inayoendana au mteja wa ISDN
kati ya watu wawili. Simu ya video
haiwezi kupigwa wakati simu nyingine ya
sauti, video au ya data inapoendelea.
1 Kuanza simu ya video, ingiza nambari
ya simu, pamoja na msimbo wa eneo.
2 Bonyeza na ushikilie kitufe cha kuita,
au chagua
Chaguzi
>
Simu ya
video
.
Kuanzisha simu ya video inaweza
kuchukua muda. Kama simu
haijafaulu, unaombwa badala yake
ujaribu simu ya sauti au utume
ujumbe.
3 Ili kukata simu, bonyeza kitufe cha
kukata simu.